Mshale wa Matumaini
Mshale wa Matumaini DOWNLOAD
Zingo na mama yake wanakimbilia ughaibuni kufuatia mzozo wa kikabila katika nchi yao. Huko ughaibuni wanakabiliwa na matatizo mengi. Zingo anafanya bidii kuyakabili licha ya umri wake mdogo. Hata hivyo, kinachomstaajabisha na kumhuzunisha ni kuhusishwa na baba yake ambaye anatuhumiwa kuwa mhalifu wa kivita.

Zingo anabaguliwa na wenzake lakini anapiga moyo konde na kuendelea na masomo yake ambayo sasa yanampa matumaini ya kuyageuza maisha yake ya karaha kuwa ya furaha. Hii ni hadithi ya huzuni inayofunua makovu ya mizozo ya kijamii hasa mizozo hiyo inavyoathiri vijana wadogo.

Profesa John Habwe ni mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Habwe ni mwandishi wa hadithi aliye na uzoefu mkubwa.